Chorus
Acheni ninyi, acheni kabisa, acheni kuwapendelea waovu
Wateteeni wanyonge na yatima, wapeni haki masikini na fukara
Waokoeni wanyonge na maskini katika makucha ya wadhalimu
Verse 2
Acheni kutoa hukumu, hukumu isiyo ya haki kwa wanyongen{Kwa kuwa (kwa kuwa) wanyonge na maskini ni wa Mungu
Msiwakandamize wanyonge kwa kuwatetea waovu } * 2
Verse 3
Lakini ninyi hamjui, aliyewapa mamlaka ni nani
Ni yeye (ni yeye) anaye uchukia uovu
Anayeuchukia uovu na kuwapenda maskini
Verse 4
Maisha ya dunia ni mafupi sana ndugu kumbukeni
Na ninyi (na ninyi) mtakufa kama wakuu wengine
Kama walivyokufa na kuyaacha madaraka na mali
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.