Chorus
Alfajiri ya kupendeza, ni siku njema sikunyenye baraka, jua limekwishachomoza,
laamsha wote waliolala, ndege naonwanalialia kumshukuru Mungu, (Njooni)
(Njooni baba mama na watoto, Njooninwote mbele za Bwana, tumtolee shukraninzetu, kwa kutoa sadaka) x2
Verse 2
Ndege wanamshukuru,
kwa sauti za kupendeza,
na sisi tumshukuru,
kwa zawadi alizotupa (Njooni)
Verse 3
Wanyama pia na mimea,
vyote vimeumbwa na Mungu,
vitu vyote vya duniani,
vyapaswa kumshukuru Mungu (Njooni)
Verse 4
Aliumba dunia hii,
kaweka giza pia mwanga,
mchana tufanyeni kazi,
usiku na tupumzike (Njooni)
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.