SectionsEucharistAmini Kuna Chakula

Amini Kuna Chakula

Marian,Ordinary TimeEucharist
Chorus

Amin, amin, nawaambieni kuna chakula kinachowafaa,

Nacho chakula ndicho kile cha uzima wa milele

Verse 2

Amin kweli, nawaambieni mwanitafuta.

Si kwa sababu mlikula ule mkate.

Si kwa sababu mliziona zile Ishara.

Bali sababu mlikula mkashiba *2

Verse 3

Msikitendee kazi chakula kinachopita.

Bali, chakula kidumucho milele.

Chakula Musa alichowapa hakiwafai,

Kweli Babangu anawapa kifaacho

Verse 4

Kile chakula chenye uzima kweli ni mimi

Ajaye kwangu hataona njaa kamwe.

Anayekula huu mwili wangu na kuinywa damu

Hukaa kwangu nami hukaa ndani yake.

Verse 5

Hicho chakula chenye uzima kweli ni mimi.

Kilichoshuka toka mbinguni kwa Baba.

Mtu akila chakula hiki hatafariki.

Bali anao ule uzima wa milele.n

Verse 6

Kile chakula ninachotoa ni mwili wangu,

Kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.

Msipokula huu mwili wake mwana Adamu.

Hamna 'zima ndani yenu.n

Verse 7

Anayekula huu mwili wangu na kuinywa damu

Ana uzima, nami nitamfufua.

Na mwili wangu ndicho chakula kile cha kweli.

Na damu yangu ndicho kinywaji cha kweli

Verse 8

Na kama Baba aliye hai 'livyonituma,

Nami ni hai, ndimi hai kwa Babangu.

Na kadhalika, mwenye kunila ana uhai,

Kweli nasema atakuwa hai kwangu,

Comments

Sign in to join the conversation

Share your thoughts on this hymn with the community.