SectionsEntranceAsiregeee Moyowe

Asiregeee Moyowe

LentEntrance
Verse 1

Asiregee moyowe, asitoke machozi

Akikumbuka Mungu wake, kwa yakenmakombozi, mtoa roho msalabani,

mtaka kufa mwenyewe, kwa sababunkumpendani, nani mfunga moyowe.

Verse 2

Bustani mle Getsemani, amwona Mungu

Baba, je mtu Mungu ana nini, nguvu zakenni haba, Bwana wangu waziona, dhambinza binadamu mwili wako umetona,

kama jasho la damu.

Verse 3

Salamu Rabi salamu, anena Yudanmbaya, mwenye moyo wake mgumu,

ambusu pasi haya aliwaambia basi,

ntakayembusu ndiye, mtwaeni na kwa upesi,

Yuda nani ni siye.

Verse 4

Yuda nani sio yeye, aliyetenda dhambi,

Tukimkosa Mungu Baba, kumdharaunnaye mwana, tukimsikitisha Roho, tunvipofu kama Yuda, tunatupa neema yake,

itokayo kwake Yesu.

Verse 5

Wote ni kupiga mbio, mitumewe pamoja,

Wamtia mikono yao, askari walokuja

Wampeleka hukumuni, aamuriwe na mtu

Atokaye uwinguni, mwanzi mkuu wa watu.

Verse 6

Mtume Petri amkanusha, amenena simjui

Uhodari umekwisha, machoye hainui

Pilato amwona Bwana, hakukosa ta neno

Asema sioni dhambi, lakini ni mwoga mno.

Verse 7

Hathubutu kumwachia, sioni nanawanmikono, mkimtaka Yesu muueni,

la mwanzi hilo neno mara askarinwamwanza, ni kupiga kelele, kumchekanna kumchokoza, mwenye mema milele

Comments

Sign in to join the conversation

Share your thoughts on this hymn with the community.