Chorus
Nimempiga shetani chenga ya mwili
Kuisalimisha roho yangu kuisalimisha roho
Nimempokea Yesu moyoni mwangu
Nipate uzima wa milele ili niishi milele
Verse 2
Tazama nimebatizwa kwa nafsi tatu
Baba mwana naye Roho Mtakatifu
Nimempokea Kristu moyoni mwangu
Kwa mwili na damu yake nimeshibishwa
Verse 3
Nimempokea Roho Mtakatifu
Amenijaza mapaji mapaji saba
Nimeikiri imani, imani yangu
Nimemkana shetani na mambo yake.
Verse 4
Nikikumbuka kiapo cha ubatizo
Najionea fahari ya ukristu wangu
Nikikumbuka ungamo la dhambi zangu
Ninaukiri upendo wa Yesu Kristu.
Verse 5
Nimeshamweka kando, shetani mwovu
Aliye mpotoshaji wa mambo mema
Alishaniweka kwenye, imaya yake
Alinidanganya sana na mambo yaken
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.