Chorus
Ee malkia wa mbingu Maria ufurahi aleluya
Amefufuka mkombozi amefufuka
Kwani mwanao uliyemchukua ametoka kaburini
Amefufuka mkombozi tufanye shangwe
Verse 2
Mauti ameyashinda Mwokozi amefufuka
Kuzimu ameshatoka Kristu na yuko hai
Shetani ameumbuka na dhambi imefutika
Verse 3
Ni kweli alivyosema ya kwamba angekamatwa
Ateswe mpaka kufa lakini angefufuka
Na sasa amefufuka ushindi tumeupata
Verse 4
Wakristu tuudumishe uhuru tuliopata
Kwa damu aliyomwaga Mwokozi msalabani
Tuache madhambi yetu tudumu katika neema
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.