Ekaristia Takatifu
Ekaristia takatifu ni mwili na damu yake Yesu
Aliyesulubiwa msalabani ili kutukomboa
Jioni Alhamisi katwaa mkate,
(Pia) Divai kawapa wanafunzi
(Ili) wanywe kwa ukumbusho wake
Njooni njooni wateule (wote)
Njooni tumwabudu Kristu katika sakramenti
(Ndugu) njooni njooni tumwabudu Yesu
Njooni njooni tumwabudu Kristu katika sakramenti
Tujongee taratibu tukale karamu takatifu
Aliyotuachia Yesu Kristu kwa ukarimu wake
Chakula cha uzima [Na] kinywaji cha roho
(Hili) ni fumbo alilotuachia
Tuadhimishe kwa ukumbusho waken
Ekaristi takatifu huleta neema ya Mbinguni,
Huleta mapatano kati yetu naye muumba wetu
Walio na imani wanayo baraka
(Hadi) milele wanalo hakikisho
(Lile) la kushiriki kwa utukufu wake
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.