Chorus
Enyi wanadamu msisumbukie maisha yenu
Kwani yale yote mnayoyasumbukia Mungu anayajuan{ Msijiulize ulize kwamba mtaishi vipi
Bali utafuteni kwanza ufalme (wa Mungu)
Nayo mahitaji yenu mnayohangaikiankila siku Mungu atawapa } *2
Verse 2
Msifikiri sana, juu ya maisha yenu
Bali mtumikieni Mungu,
Kwa kusali na kutenda mema,
Kwa kuwa Mungu ndiye mtoaji wa vyote
Verse 3
Jueni Mungu ndiye, kinga ya maisha yenu
Sasa mtumikieni Mungu,
Kwa kusali na kutenda mema,
Kwa kuwa Mungu ndiye mtoaji wa vyote
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.