Chorus
{We Maria
Umebarikiwa kuliko wanawake wote
Umetuzalia Mtoto Mwanaume } *2
Mwenye ufalme mabegani mwake * 2
Verse 2
Bikira Maria umebarikiwa kuliko wanawake wote
Umetuzalia mtoto mwanaume, mtawala ni mfalme wetu
Verse 3
Mtoto mwanaume ni Bwana mtawala wa Mbingu na dunia
Maria ni Mama, ni Mama wa Mungu, pia ni mama yetu sisi
Verse 4
Ee Mama wa Mungu tunakupongeza kwa kutuletea Mwokozi
Maria twaomba maombi yetu yafike kwa Yesu mwanao
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.