Chorus
{ Fadhili za Bwana zina wamchao
Tangu milele hata milele } *2
Verse 2
Ee nafsi yangu umhimidi Bwana
Naam vyote vilivyo ndani yangu
Vilihimidi Jina lake tukufu
Verse 3
Akusamehe maovu yako yote
Akuponye magonjwa yako yote
Aukomboa uhai wako na kaburi
Verse 4
Bwana ndiye afanyaye mambo ya haki
Na hukumu kwa wote walioonewa
Alimjulisha Musa njia zake
Verse 5
Bwana amejaa huruma na neema
Haoni hasira ni mwingi wa fadhili
Hakututenda sawa na hatia zetu
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.