SectionsExitFuaha Yako

Fuaha Yako

Ordinary TimeExit
Chorus

Kuna kitu wewe wawaza

(na pia) kuna kitu wewe wapenda

(Tazama) kuna kitu wewe watakandaima mchana usiku wawaza

(Na sasa) ukipata unafurahi

(kuliko) nazo shida kuzisahau

(Tazama) moyo hujawa na furahanna kumbe matatizo unaongeza

Chorus

Ukienda huku we - barabara ni yako we

Ukirudi huku lo - barabara ni yako tu

Kwenye kuongea we - tunajua ni wewe tu

Na kwenye kelele -tunajua ni wewe tu

Ukienda huku we - mbele kweli yako we

Ukirudi huku lo - katikati chako we

Ukienda kule ee - na ulafi ni wako we

Ukifurahia ee - nayo gongo ni yako eh!

Unachokijua kimoja - ulevi,

nyumba imekuwa ni fujo,

(Tazama) Kelele huzuni na kero,

sababu ya kukarabati mizigo

(Najua) kazi hiyo aliyekupa ni nani,

shetani mpenda tamaa

(Huoni) amani upendo huruma hakuna,

huwezi kupata furaha

Verse 3

[s]

Unapokipata kinywaji, kazi yako wewe ni moja

Wenzako wakipata kiu, wewe unamiminia

Furaha yako iliyoje, kujiburudisha na pomben[b]

Itazame na afya yangu, na sasa inayo migogoro

Chakula kwangu siyo kitu, pombe na mimi mimi na pombe

Hata na maendeleo yangu yamekuwa ni ya kuzorota

Verse 4

Itazame na nyumba yetu, amani upendo hakuna

Watazame watoto wetu, afya yao inavyoyumba

Nguo zao sasa ni duni, viraka vina mkutano

Nikitazama ndoa yangu, ni lawama na ni lawama

Kurudi kwangu ni usiku, tena usiku wa maneno

Nina shtuma kama shindano, huyu maarufu gani tena?

Verse 5

Uurudishe moyo nyuma, ukabadilike mwenendo

Familia uitazame, ndoa nayo uijali

Watoto msingi wa kesho, maendeleo wajengee

Kumbe kweli nilipotea, na kuyasahau majukumu

Familia hata ndoa yangu, nilitelekeza kwa ulevi

Hata na mlango wa kanisa na jumuiya sikukumbuka

Comments

Sign in to join the conversation

Share your thoughts on this hymn with the community.