Je! Je! Ni nani aliyesadiki habari hii tuliyoleta
Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani
Maana alikua mbele zake kama mche kama mche mwororon(Na kama) kama mzizi katika nchi kavun{ Alidharauliwa na kukataliwa na watu
Mtu mwenye huzuni nyingi ajuaye sikitiko } *2
Ni kama mtu ambaye watu humficha uso
Aliyedharauliwa, hakuhesabiwa kitu
Hakika kayachukua, na masikitiko yetu,
Amejitwika huzuni, huzuni, huzuni yetu
Lakini tulidhania, yeye kuwa amepigwa
Ya kuwa yeye kapigwa kapigwa yeye na Mungu
Bali alijeruhiwa, yeye kwa makosa yetu
Alichubuliwa yeye, pia kwa maovu yetu
Adhabu amani yetu, ilikuwa juu yake,
Kwa kupigwa kwa sisi, sisi sote tumepona
Sisi ni kama kondoo, kondoo tumepotea
Tumegeukia njia, kila mtu njia yake
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.