Verse 1
{ Bwana harusi na bibi harusi, leo mmefunga ndoa ya maisha,
Kaeni kwa amani kidededede } * 2
Chorus
Upendo wenu umedhihirika
Uyani kwenu bamba ishini tototo
Uzuri wenu hauna kifani
Uyani kwenu bamba ishini tototo
Na nyumba yenu imebarikiwa
Uyani kwenu bamba ishini tototo ooo
Verse 3
Jitulize mjisikie sukari, siku ya leo ni yenu,
Furahini, mmepambwa maua mnapendeza
Verse 4
Bwana arusi kwanza wachangamka, bibi arusi chachawa,
Chezacheza, penzi lenu leo limekamilika
Verse 5
Mapenzi yenu yote yatasitawi, hakika yatasitawi,
Yatamea, kama ule mwerezi wa Lebanoni
Verse 6
Baraka zake Mungu ziwashukie, kaeni pasipo shida,
Siku zote nyumba yenu iwe hekalu la Mungu.
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.