Hiki ni chakula kwa wote wampendao
Mkate na divai ni chakula cha Roho
Wanyofu wa moyo twendeni tukampokee
Tupate uzima wa milele na milele
Bwana Yesu alhamisi kuu kajitolea,
Mwili na damu yake ziwe kiburudisho
Akatuamuru tukipenda kumkumbuka,
Mwili na damu ni ishara ya penzi lake
Alaye mwili na kunywa damu asema Bwana
Aishi ndani yangu na mimi ndani yake
Yeye ni rafiki yangu na nitamfufua,
Nitaandamana naye safarini mwake
Alaye mwili wa Yesu na kuinywa damu,
Bila stahili ana hukumu ya milele
Tujitakase kabla ya kula karamuyo,
Kitubio ni sakramenti ya mapatano
Ee Yesu nipe neema ya kukupokea,
Unipe nguvu ya kuweza kujitakasa
Unijalie kukupenda na moyo wote,
Mwishowe nishiriki karamu ya Mbinguni
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.