Chorus
Ishara kubwa imeonekana Mbinguni *2n{ (Ambapo) mwanamke aliyevikwa jua
Pia na mwezi chini ya miguu yake
Na taji la nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake } *2
Verse 2
Tufurahie sote katika Bwana, tunapoadhimisha
Siku kuu kwa heshima ya Bikira Maria
Verse 3
Jeshi la malaika washangilia, pia wafurahia
Kupalizwa Mbinguni kwake Bikira Maria
Verse 4
Bwana amefunua wokovu wake, kati ya mataifa
Ameidhihirisha haki yake juu ya nchi
Verse 5
Atukuzwe Baba pia na Mwana, na Roho Mtakatifu
Kama mwanzo sasa na siku zote na milele
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.