Chorus
Bwana jahazi letu, kweli laangamian{Mawimbi yametuzidia jahazi ladidimia} *2
Wale papa na nyangumi wataka watumeze sisi
Verse 2
Jahazi, jahazi we!
Jahazi limejaa mizigo ya dhambi na chuki
Ewe Bwana tuondolee jahazini kwa kweli
Verse 3
Jahazi, jahazi we!
Jahazi lina masengenyano fitina inapatikana we!
Tuondolee jahazini kwa kweli
Verse 4
Jahazi, jahazi we!
Jahazi lako Bwana nataka lenye uzima wa milele
Ni jahazi la neema kwa kweliJA
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.