Chorus
Waambieni watu walio na moyo wa hofu *2n{ Jipeni moyo, msiogope (ogope) [kwa maana]
Tazama Mungu wenu nakuja kuwaokoa nyinyi } *2
Verse 2
Itieni nguvu mikono iliyo dhaifu
(Na fanyeni imara magoti yaliyolegea *2)
Verse 3
Ndipo macho ya vipofu yatafunguliwa
(Na masikio ya viziwi yatazinduliwa *2)
Verse 4
Ndipo na kilema atarukaruka
(Na ulimi wake bubu ndipo utakapoimba *2)
Verse 5
Na katika nyika maji yatabubujika,
(Na nchi yenye kiu itakuwa chemichemi *2)
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.