Kipeperushe Kitamba Chako
[ t ] Jiangalie jinsi unavyoenenda,
ujiulize kama hivyo ni sawa
Ndugu rejea ahadi yako kumkataa Ibilisi muovun[ t ] Dhamira yako inakuambia nini,
inakusuta au bado ni huru, sasa
Ndugu rejea ahadi yako kumfuata Bwana Yesu milele
Ewe Mwenzangu - kipeperushe kitambaa chako
Cha ubatizo - cheupe kinachomeremeta
Kisichafuke - kipeperushe kitambaa chako
Cha ubatizo - cheupe kinachomeremeta
Kiweke safi - kipeperushe kitambaa chako
Cha ubatizo - cheupe kinachomeremeta
Uliye naye kweli ni mzuri sana,
pia kumbuka yuko wako wa ndoa -
Uliyeapa ni wewe sio mwingine,
kushikamana naye yule mmoja, basi -
Maendeleo kweli ni muhimu sana,
lakini na wenzako wanahitaji -
Hicho kipato ndicho ulichopimiwa,
au mwenzetu unachota zaidi, leo -
Unatamani kuwa mwenye madaraka,
umejiandaaje kuyatumia -
Je ni halali watu tukakutukuza,
wakati yupo yule alokuumba, haya -
Kumbuka Yesu alipigwa mijeredi,
kwa sababu ya haya unayotenda -
Akatundikwa mtini akiwa tupu,
kadhalilishwa mwisho akauawa, hivyo -
Kumbuka kuwa siku ile inakuja,
matendo yako yote kuhesabiwa -
Ni heri leo ukitunze kitambaa,
siku ya mwisho kiwa bado cheupe, kweli -
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.