Chorus
Bwana ee Bwana, kwa nini wasimama mbali
Ee Bwana ee Bwana, kwa nini wasimama mbalin{ Kwa nini kujificha na kujificha nyakati za shida
Kwa nini kujificha Bwana nyakati za shida } *2
Verse 2
Kwa kiburi chake mtu asiye haki
Mnyonge anafuatiwa anafuatiwa kwa ukali
Na wanaswe kwa hila hizo hizo walizoziwaza
Verse 3
Maana mdhalimu, mdhalimu hujisifia
Hujisifia sifia tamaa ya nafsi yake
Na mwenye uchoyo humkataa Bwana na kumdharau
Verse 4
Asema moyoni mwake, asema sitaondoshwa
Kizazi hata kizazi, sitakuwamo taabuni
Kinywa chake kimejaa laana na hila na dhuluma
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.