SectionsEntranceKwa Nyimbo Nzuri

Kwa Nyimbo Nzuri

Marian,Ordinary Time,BaptismEntrance
Verse 1

Kwa nyimbo nzuri za furaha,

njooni nyote mbele za Bwana

Kwa shangwe na vigelegele,

tumwimbie Mfalme wetu

Chorus

Mataifa yote simameni mbele zake Bwana,

Makabila yote njoni leo nazo ngoma zenu

Chezeni mbele za Bwana!n{ Wajaluo na waimbe nyimbo

Wamasai na waruke juu

Wabaluhyia na wapige ngoma

Wakikuyu na wacheze sana,

Watu wote sisimukeni,

Shangwe nderemo na kelele, pigeni makofi } *2

Verse 3

Vinanda vifijo kelele,

makofi machezo nderemo

Kusifu kweli kwawapasa,

enyi wanyofu wa moyo

Verse 4

Pigieni Mungu kelele,

imbeni utukufu wake

Tukuzeni sifa za Mungu,

tangazeni matendo yaken

Verse 5

Shukuruni Bwana kwa zeze,

kwa kinanda cha nyuzi kumi

Mfanyieni Bwana shangwe,

mtumikieni kwa furahan

Comments

Sign in to join the conversation

Share your thoughts on this hymn with the community.