Chorus
Leteni ndama walionona madhabahuni kwa Bwana tena
Toeni bila kinyongo moyoni ndipo mtabarikiwa naye * 2
Verse 2
Leteni ndama aliyeshiba majani ya kondeni,
mkamtolee Mungu Baba yenu kwa shukrani.
Verse 3
Peleka sadaka yako iliyo safi na ya kupendeza,
ndipo utakapokitikisa kiti cha mwenyezi.
Verse 4
Kumbuka yule mjane aliyetoa senti moja,
alibarikiwa na kuongezewa na mwenyezi.
Verse 5
Sadaka iliyo safi ni ile inayokugusa wewe,
hiyo ndiyo sadaka iliyo safi sana.
Verse 6
Isaka alitolewa na baba yake kama sadaka,
hivyo Abrahamu alizidishiwa uzao wake.
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.