Maajabu Ya Mungu
Maajabu ya Mungu kaumba watu wa rangi mbalimbali *4
Wengine ni weusi, wengine ni weupe,
Wengine ni wekunde, wengine ni wekundu,
Wote ni wa Mungu, wote
Maajabu ya Mungu kaumba watu wa kimo mbalimbali *4
Wengine ni warefu wengine ni wafupi,
Wengine ni wanene, wengine ni wembamba
Wote ni wa Mungu, wote
Maajabu ya Mungu kaumba watu wa wito mbalimbali *4
Wengine ni wa ndoa, wengine ni watawa,
Wengine makuhani, wengine ni wa ndoa
Wote ni wa Mungu, wote
Maajabu ya Mungu kaumba watu wa kazi mbalimbali *4
Wengine makarani, wengine ni polisi
Wengine waalimu, wengine makarani
Wote ni wa Mungu, wote
Maajabu ya Mungu kaumba watu wa umri mbalimbali *4
Wengine ni watoto, wengine ni vijana,
Wengine ni wa kati, wengine ni wazee
Wote ni wa Mungu, wote
Maajabu ya Mungu kaumba watu wa sifa mbalimbali *4
Wengine ni hekima, wengine ni busara,
Wengine polepole, wengine ni haraka
Wote ni wa Mungu, wote
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.