Majibu Ya Msalaba
Nimejua waziwazi yanapotoka haya,
Na ninayoyatafuta usiku mchana
Yanatoka kwa kiasi na kiwango kamili
Kwa wakati ufaao na lugha sahihi
Yamepita kimo changu cha kuyatafakari
Yana raha mwisho wake machungu mwanzonin{ Yaone, hayakujificha, kabisa, yamefunuliwa
Kwa yule, aliyefunuka, aliye, moyo wazi ae }*2
Nimeyaona, nimeyatambua!
{ Majibu majibu he!
Yanatoka pale kwenye msalaba juu }* 2n{ Kimbilio-nah ah aeeh msalaba huu wa Yesu
Tumaini-nah ah aeeh msalaba huu wa Yesu } *2
Kujua kujizuia yale yenye unono
Kujua kuyapokea yale machungu chungu
Kukubali kupokea hasara bila kosa
Kusudi kumsamehe yule aliyekosa
Kukabidhi maumivu kwa Yesu bila shaka
Na kuacha kupanga majibu na muda wake
Kuamini bila mwisho ingawa sijaona
Kutumaini ya kwamba Yesu aweza yote
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.