Mama Pale Msalabani {Alternative}
Mama pale msalabani, macho yatoka machozi
Akimwona mwanaye, akimwona mwanaye
Kweli vile akilia, uchungu kama upanga,
Ukampenya moyowe, ukampenya moyowe
Mwenye moyo mgumu, nani asimhurumie basi
Mama mlilia mwana, mama mlilia mwana?
Ewe mama mtakatifu, usulubiwe na Yesu
Moyo wangu mwenye dhambi, moyo wangu mwenye dhambi
Naye Mwokozi niteswe, na madonda nigawie
Pamoja na ukombozi, pamoja na ukombozi
Nisimame msalabani, niwe nami wako mwenzi
Wa uchungu na msiba, wa uchungu na msiba
Nisianguke motoni, uniwie msimamizi,
Ewe Bikira mwema, ewe bikira mwema
Msikilize mama yako, niponye siku ya mwisho
Ewe Mwokozi wangu, ewe Mwokozi wangu
Nitakapokufa mimi, upokee roho basi
Niende kwako Mungu, niende kwako Mungu
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.