SectionsEucharistMchunga Wangu

Mchunga Wangu

Ordinary Time,Ordinary TimeEucharist
Chorus

Mchunga wangu ameniandalia mema yote.

Verse 2

Bwana ndiye mwenye kuchunga uzima wangu,

na malisho yangu kwangu ni raha milele.

Malishoni mwake mabichi ananilaza,

sitakosa kamwe, wala sitapungukiwa.

Penye maji yake mazuri ya utulivu, ndiponkweli Mungu anaponiburudisha

Ananiongoza pasipo mashaka yeye,

penye njia zake nzuri, adili na nyofu

Katika mabonde ya uvuli wa mauti,

na(a)m ninapopita, sitaogopa mabaya.

Kwa maana wewe upo pamoja na mimi,

gongo lako na fimbo yako vyanifariji.

Waniandalia vitamu mezani mwako,

nami nitashiba mbele za watesi wangu.

Na kichwani pangu mafuta ukanipaka,

na kikombe changu kweli chajaa memayo

Wema na fadhili za Bwana zimenijia,

kwa maisha yangu, mpaka niage dunia.

Ninaomba kwake mchungaji wa roho yangu,

na nikae kwake, mpaka nyakati za mbali.

Comments

Sign in to join the conversation

Share your thoughts on this hymn with the community.