Milele Milele Msifuni
Easter,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary TimeThanksgiving
Verse 1
Milele milele msifuni Bwana
Na ahimidiwe Bwana milele,
Amina, amina, aleluya
Rehema za Bwana ni za milele
Na uaminifu wa Mungu wetu,
Ni kwa vizazi hata vizazi
Chorus
{ Njooni, tuimbe, tumwimbie Bwana
Yeye (ndiye) wokovu, wokovu wetu (Bwana)
Ni Mungu wetu na mwumba wetu, aleluya aleluya } *2
Verse 3
Nitakushukuru ee Bwana Mungu
Nitalishukuru jina la Bwana,
Ee Bwana mfalme Mungu wangu
Pigeni vigelegele pigeni
Pigeni magoti mbele za Bwana
Kwa maana ndiye Mungu wetu
Verse 4
Atawabariki wamchao Bwana
Wadogo wakubwa awabariki
Msaada wao na ngome yao
Tazama atabarikiwa hivyo
Atabarikiwa amchaye Bwana
Awabariki toka Sayuni
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.