Chorus
{ Mimi ndimi mzabibu wa kweli,
Mimi ni mzabibu wa kweli
Nanyi m matawi yangu, asema Bwana } *2
Verse 2
[ b ] Na Baba yangu ndiye mkulima,
Kila tawi lisilozaa, Baba hulikata
Nalo tawi lizaalo, Baba hulisafisha, ili lizidi kuzaa
Verse 3
Kaeni nyote ndani yangu mimi,
Nami nikae ndani yenu, kwa maana mtu
Akaaye ndani yangu, nami ndani yake, huyo huzaa matunda
Verse 4
Mimi ni mti mti wa zabibu,
Nanyi ndinyi matawi ya mzabibu huu
Tawi linalojitenga, kutoka kwa mti huu, hunyauka tena hufa
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.