Mimi Nimeumbika
Easter,Easter,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary TimeThanksgiving
Chorus
{ Mimi oh! oh oh! mimi oh! oh oh!
Niumbika mimi kweli napendeza } *2n{ Nitakuimbia, nitakuchezea
Asante Baba kuniumba jinsi nilivyo } *2
Verse 2
Nampenda Bwana kwa kuwa ananisikiliza
Huisikiliza sauti yangu na dua zangu
Hunitegea sikio lake nimwitapo yeye
Kwa hivyo nitaliita jina lake siku zote
Verse 3
Kamba za mauti ziliponizunguka mimi
Shida za kuzimu zikaniandama sana
Niliona tabu nyingi nikamlilia Bwana wangu
Nami nikaliita jina lake akaniokoa
Verse 4
Bwana katujalia sauti nzuri ya kupendeza
Ili tumwimbie yeye siku zote maishani
Kwa hivyo yatupasa sote kumwimbia yeye
Kwani Mungu wetu ni mkarimu kwa watu wote
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.