Chorus
{ Mimi nimewachagua ninyi duniani
Mimi nimewachagua duniani } *2n{ Ili mpate kwenda kuzaa matunda
Na matunda yenu yadumu, yadumu, siku zote } *2
Verse 2
(Yesu alisema) si ninyi mlionichagua mimi,
Bali ni mimi nimewachagua ninyi
Verse 3
Nami nimewaweka kwenda kuzaa matunda
Na matunda yenu yadumu
Ili kwamba lolote mumwombalo Baba
Kwa jina langu awapeni
Verse 4
Iwapo ulimwengu utawachukia
Mjue kwamba umenichukia miminkabla ya kuwachukia ninyi.
Verse 5
Kama mngekuwa wa ulimwengu,
Ulimwengu ungeliwapenda
Lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu,
Bali mimi nimewachagua katika ulimwengu,
Kwa sababu hiyo ulimwengu utawachukia.
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.