SectionsEucharistMisa Kiserian (Utukufu)

Misa Kiserian (Utukufu)

Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Ordinary TimeEucharist
Chorus

Utukufu kwa Mungu juu mbinguninna amaninna amani

Duniani

Duniani kwankwa watu wenye mapenzi mema

Verse 2

Tunakusifu, tunakuheshimu,

twakuabudu, tunakutukuza

Twakushukuru, mfalme wa Mbinguni,

kwa ajili ya utukufu wako.

Verse 3

Ee bwana Mungu, Mfalme wa mbinguni,

Baba Mwenyezi, Muumba wa wote

Ee Bwana Yesu, Mwana wa pekee

Mwana kondoo, Mwana wake Mungu.

Verse 4

Uondoaye, dhambi za dunia,

tuhurumie, utuhurumie

Uondoaye, dhambi za dunia,

ulipokee, hili ombi letu.

Verse 5

Unayeketi kuume kwa Baba tuhurumie,

utuhurumie, Kwa kuwa wewe,

ndiwe peke yako, Mtakatifu,

peke yako Bwana

Verse 6

Peke yako mkuu, Bwana Yesu Kristu,

pamoja naye, Roho Mtakatifu

Kwa utukufu, wake Mungu Baba,

milele yote, Amina, Amina

Comments

Sign in to join the conversation

Share your thoughts on this hymn with the community.