SectionsExitMizinga Maroketi

Mizinga Maroketi

Ordinary TimeExit
Verse 1

Amani ya dunia imetoweka

Tumuombe Mwenyezi aturudishie

Tamaa ubinafsi vilivyoshamiri

Ni sumuyo amani tunayohitaji

Chorus

{

Aa-eh njooni wote

Aa-eh tusali pamoja

Aa-eh tuombee amani

Hatari inatukabili

Tumuombe Mungu atuepushen} * 2

Verse 3

Mizinga maroketi imetayarishwa

Madege ya kutisha ituangamize

Ngao yetu wanyonge ... ...

Yatubidi tusali vita tutashindan

Verse 4

Ujambazi wa kutisha umetuandama

Mali yathaminiwa kuliko uhai

Twahitaji ulinzi wa Mungu Mwenyezi

Aombaye hupewa, njooni tuombe

Verse 5

Ndani ya familia moto unawaka

Kupigwa tusi mateke sasa ndizo sala

Watoto nao pia ni vurugu tupu

Hawana mchungaji kwenye familia

Verse 6

Wito umetolewa tusali rozari

Baba Mtakatifu anatuhimiza

Matendo ya rozari tuyatafakari

Naye Mama wa Mungu atatusikia

Comments

Sign in to join the conversation

Share your thoughts on this hymn with the community.