Moyo Wangu Wamtukuza
Moyo wangu wamtukuza Bwana, Rohonyangu inafurahi x2
Kwa kuwa amemwangalia
Kwa huruma mtumishi wake
Hivyo tangu sasa watu wote
Wataniita mwenye heri
Kwa sababu mwenyezi Mungu
Amenifanyia makuu
Jina lake ni takatifu
Huruma yake ni kwa wote
Wote wale wanaomcha
Kizazi hata na kizazi
Huyatenda mambo makuu
Kwa nguvu za mkono wake
Wenye kiburi hutawany
Hushusha wote wenye vyeo,nkutoka vitini vya enzi,
Nao wote wanyenyekevu,nwote hao huwainua
Huwashibisha wenye njaa,nna matajiri huwaacha,
Waende mikono mitupu.
Hulilinda taifa lake, teulenna mtumishi wake,
Kikumbuka huruma yake
Kama alivyo waahidia,nbabu zetu kawahidia,
Ibrahim na uzao wake.
Atukuzwe Baba na Mwana,nnaye Roho Mtakatifu,
Leo, kesho hata milele,nkwa shangwe milele amina.
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.