Moyo wangu wa mwadhimisha Bwana
Roho yangu yamfurahia Mungu
Ni kwa kuwa ameutazamanunyonge wa mjakazi wake
Kwa maana tazama tokea sasa
Vizazi wataniita mbarikiwa
Kwa kuwa amenitendea mambo makuu
Na jina lake takatifu kweli
Ameyatenda maajabunna jina lake takatifu
Wamchao hudumisha rehema
Vizazi hata na vizazi
Amefanya nguvu kwa mkono wake
Atawanya wote wenye kiburi
Aangusha wakuu wa enzi
Na wanyonge yeye huwakweza
Wenye njaa amewashibisha mema
Walio na mali aondoa tupu
Amemsaidia mtumishi wake
Ili kukumbuka rehema zake
Utukufu kwao Baba na Mwana
Msaada wa Roho Mtakatifu
Kama ulivyokuwa hapo mwanzo
Ni vivyo sasa hata milele
Utukufu kwa Baba na Mwana kwa Roho
Kama vile mwanzo wa hata milele Amina
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.