Msinyamaze
Ni vyema sana kumwimbia Bwana
Kusifu kwapendeza ni kuzuri (ni kuzuri)
Ni vyema sana kumwimbia Bwana
Kusifu kwapendeza ni kuzuri, (ni kuzuri sana)
Kumfanyia shangwe nyimbo na zaburi
Kusifu kwapendeza ni kuzuri, kabisa
Fanyeni kanuni moja wapendwa
Kwenu kumwimbia Mungu wenu daima
Maana aliwapeni sauti na vinywa
Hivyo kumwimbia Mungu wenu ni vyema
Ni vyema sana kumwimbia Bwana
Kusifu kwapendeza ni kuzuri, kabisa
Funueni vinywa vyenu wapendwa
Kwani kumwimbia mungu wenu ni herinkwa kuwa amepita sifa zote za vinywa
Bali kumwimbia Mungu wenu ni vyema
Ni vyema sana kumwimbia Bwana
Kusifu kwapendeza ni kuzuri, kabisa
Kuimba msiache msinyamaze
Hata mtokwe jasho msinyamaze
Vijana na wazee msinyamaze
Watoto himahima msinyamaze iyelee
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.