Ndugu yangu sikia nasema kwa makini,
Habari hii kuu ya ufalme wa Mungu
Inasikika sana, sasa imeenea,
Lakini sio wengi, wanaoiamini
Waimbaji tumeshaimba nyimbo nyingi
Makasisi wamehubiri pande nyingin{ Twasema uokoke, nawe wasema kesho
Inapofika kesho, wasema kesho kutwa
Siku nazo zapita, miaka inapita
Uchague mwenyewe, Mungu au shetani } *2
Ukizipata shida, walaumulaumu,
Ndugu na majirani, wadhani umelogwa
Unaanza ugomvi, wachukia wengine,
Hata bila sababu wawaita wachawi
Waomba mara moja, ukikosa majibu,
Kesho inapofika waenda kwa mganga
Ngoja nikueleze, Mungu hana haraka,
Jifunze vumilia majibu utapata
Jifikirie ndugu, usingoje ya kesho,
Muda ni wako sasa, amua ukubali
Mengi tumeyasema, ilobaki ni kwako,
Uchague mwenyewe, Mungu au shetani
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.