Chorus
Enyi watumishi wa Bwana sifuni
Lisifuni lisifuni Jina la Bwana
Na ahimidiwe Bwana Mungu
Bwana Mungu kutoka Sayuni
Akaaye Yerusalemu aleluya
Verse 2
Ninyi msimamao nyumbani mwa Bwana
Nyuani mwa nyumba ya Mungu wenu
Msifuni Bwana kwa kuwa yu mwema
Liimbieni jina lake kwa maana lapendeza
Verse 3
Kwa sababu Bwana amejichagulia Yakobo
Na Israeli wawe watu wake hasa
Maana najua mimi ya kuwa Bwana ni mkuu
Na Mungu wetu yu juu ya miungu yote
Verse 4
Enyi mlango wa Israeli mhimidini
Enyi mlango wa Haruni mhimidini
Enyi mlango wa Lawi himidini Bwana
Enyi mnaomcha Bwana mhimidini Bwana
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.