Verse 1
Naondoka mimi naenda kwa Baba,
Nipeleke hiki nilichokipata,
Japo kidogo, sitaona haya,
Nimeamua, sitarudi nyuma
Chorus
{ Nakuja polepole Baba,
Nakuja na zawadi yangu
Naleta mbele zako ili nitoe shukurani } *2
Verse 3
Natembea mimi mwendo wa madaha,
Nakanyaga chini kwa maringo tele,
Naelekea, altare ya Bwana,
Nimkabidhi, nilichojaliwa.
Verse 4
Nimechangamka ninashangilia,
Napiga kelele kelele za shangwe
Nachezacheza, najongea kwako,
Ee Mungu Baba Nipokee mimi.
Verse 5
Nafsi yangu mimi naileta kwako,
Mkate divai pia ninaleta
Uigeuze, mwili na damuyo,
Chakula chetu, tunaosafiri
Verse 6
Mavuno shambani mimi nimevuna,
Mifukoni fedha nimekabidhiwa,
Mimi ni nani, nisikushukuru,
Baba nasema asante kwa yote.
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.