Nasikia Sauti Nzuri
Nasikia sauti nzuri kama ya malaika
Ni sauti toka mbinguni, sauti ya Mungu
Aniita mimi niende nikamtumikie
Anitume shambani mwake nikavune yote
Umeniita, nimeitika wito, nakuja kwako leo,
najongea mbele zako Bwana nipokee mimi,
niko tayari, nimeyaacha yote,
najikabidhi kwako,
unitume popote nami nitakwenda haraka
Ninaenda mimi naenda, ninaenda mwenyewe,
ninaenda mbele za Bwana, sitarudi nyuma,
ndugu zangu na marafki, mniache niende,
nikafanye kazi ya Bwana, nitakapotumwa
Nilitazama moyo wako, moyo wako mwanangu,
hata kabla hujazaliwa, nilikutambua,
nilikuteua mapema kati ya ndugu zako,
uwe kuhani wangu mimi, kuhani mkuu
Shamba lake Bwana ni kubwa nanmavuno ni mengi,
wavunaji ndio wachache nitakwenda mimi,
nakuomba sana ee Bwana,
nipeleke shambani,
nikavune mavuno yote yaliyo tayari.
Uwe nami siku kwa siku, Bwana usiniachenunikinge na majaribu nilinde daimannipeleke habari njema, ulimwenguni mwote,
watu wote wakutambue, wakugeukie
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.