Nipishe njia nipeni nafasi
Nimuonyeshe Mungu nilivyofurahi
Nitamwimbia ngoma nitacheza
Nimuonyeshe Mungu nilivyofurahi
Natamani kuruka, nifika kule
Nimuinue Mungu kwa mikono yangu
Nimueleze kwa kinywa, changu mwenyewe
Kwamba nimefurahi kwa upendo wake
Bwana nashukuru, nashukuru nashukuru tu
Ninashukuru kwa kunipenda bila mwisho
Sina cha kusema, cha kusema cha kusema tu
Ninashukuru kwa kunipenda bila mwisho
Kaniinua kutoka shimoni -
Akaniweka juu ya kinara -
Nitazunguka kwa maringo tele -
Na tabasamu lisilo kauka -
Nitawashika wenzangu mikono -
Tujiinue juu kwa pamoja -
Wenzangu si mmejionea wenyewe -
Mungu alivyo mwema wa ajabu -
Nitaandika utukufu wake -
Na wajukuu wangu wausome -
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.