Verse 1
Nimekukosa Bwana, kwa moyo wote ninajuta kweli, kwa moyo wote
Roho yangu ina-yohuzunika ninapokuona ulivyokufa
Chorus
{ Natazama Kalvari (Bwana) ulivyotundikwa mtini (kweli)
Mwili wangu wanyong'onyea ulivyosulibiwa } *2
Verse 3
Tena ni mimi Bwana, ni dhambi zangu ulizozifia, msalabani
Kifo cha aibu, kilikufika makusudi mimi, niokolewe
Verse 4
Kwenye kilima kile, walikusonya wakisema wote, asulibiwe
Kifo chako kwetu ni ukombozi wa mioyo yetu, na roho zetu
Verse 5
Unitulize Bwana, kwa mkono wako kwani ninatubu, makosa yangu
Naanguka kwako kifudifudi, ninaomba toba, kwa moyo wote
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.