Niko Tayari Kuhubiri Injili
Niko tayari kuhubiri injili, niko tayari niko tayari
Mahali popote na wakati wowote, niko tayari niko tayari
Niko tayari kuitangaza neon, neno la Mungu kwa mataifa,
Mungu Mwenyezi niwekee mikono, nikahubiri nikahubiri
Ninakutegemea Mungu Mwenyezi, ukanilinde uniongoze
Utume na Roho Mtakatifu, akanijaze niwe imara
Nikahubiri bila kuwa na woga, wakasikie dunia yote
Niwaamshe wote walio walala, niwaelekeze kwa Mungu wetu
Niwape nguvu na waliolegea, na wazipate wawe imara
Na wale wote wakisikia neon, walisikie na watambue
Ninawaomba waumini wenzangu, mkanipe ushirikiano
Na mema yote nitakayofundisha, mkayashike na kuyaishi
Na waalika wote tukahubiri, tukahubiri neno la Mungu
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.