Nikupe Nini Ee Mungu
Nikupe nini ee Mungu cha kukupendeza
Uwezo wangu mdogo Bwana waujua
Pamoja na dhiki inayonisonga
Pokea zawadi yangu hii duni
Nikitazama wenzangu wanakutolea
Zawadi nyingi na nzuri za kukupendeza
Kasoro mimi tu natoa kidogo
Wakati mwingine sitoi kabisa
Maisha yangu ya dhiki Bwana wayajua
Unyonge na udhaifu wangu waujua
Sina kitu mimi cha kukutolea
Lakini pokea nafsi yangu Bwana
Nayakabidhi maisha yangu kwako Bwana
Uniongoze katika njia za uzima
Unisaidie wakati wa shida
Kwani ni wewe tu tumaini langu
Kutoa ndugu ni moyo sio utajiri
Ukimtolea Mungu atakuongeza
Uwasaidie watu maskini
Wasiojiweza utabarikiwa
Ninawasihi wenzangu mliojaliwa
Maisha bora mazuri na ya kuridhisha
Msimsahau Bwana Mungu wenu
Toeni kwa wingi mtabarikiwa.
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.