Nimemkataa Shetani
Je je, umemkataa shetani huyo na mambo yake yote
Nimemkataa shetani na vishawishi vyake vyote
Je je, umemkataa shetani huyo na ila zake tamu
Nimemkataa shetani na mazingaombwe yake
Mtazame huyo mwovu na chengachenga zake,
Huja pole pole,mwenye stara zake,
malaika wa mwangaza yuaja kunizuzua
Bwana ninakuomba macho nifungue,
nipate kuyajua, mema na mazuri,
ya ufalme wako, niyaache ya shetani
Mungu kaniinua, kanitoa kwenye shimo,
alimokua yule mwovu kanitia pingu,
sasa niko huru, ninatabasabu,
nitamuinua nitasema mimi nimemkataa shetani
Sina hofu mimi,sina haya kumsifu,
aliyeshinda vita hivyo sasa mimi mzima,
nami nitafuata,
jia zake hata,
mwisho wa dahari ama kweli mimi nimemkataa shetani
Chenga chenga zake,n imeasi tena sana,
majaribun hayo sina budi kuyahepa mimi,
nitaishika kweli Imani sitakubali anishinde mimi nimemkataa shetani.
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.