Nimeonja Pendo Lako
Nimeonja pendo lako, nimejua u mwema
Nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe
Nitawaongoza vyema waimbe kwa furaha
Nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe.
Ukarimu wako Bwana, na huruma yako wewe
Msamaha wako Bwana, na upole wako (wewe)
Umenitendea wema usiopimika
Nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe
Kina mama simameni, piga vigelegele
Na kina baba nyanyuka mkapige makofi
Watu wote nesanesa chezeni kwa furaha
Inua mikono juu, mshangilieni Bwana
Watawa washangilie, makasisi waimbe
Walei warukeruke, waseme aleluya
Vitambaa mikononi, vipeperushwe juu
Na vichwa viyumbeyumbe kwa mwendo wa kuringa -
Nitakushukuru mimi, na nyumba yangu yote -
Nitayatangaza haya, maisha yangu yote -
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.