SectionsEucharistNinakupenda Ewe Mwokozi

Ninakupenda Ewe Mwokozi

Ordinary Time,MarianEucharist
Chorus

Ninakupenda ewe Mwokozi wangu,

rafki yangu mpenzi wa moyo wangu,

Ukae nami daima ndani yangu,

nipate nguvu na heri siku zote.

Verse 2

Nina kutolea mwili na roho yangu,

unipe neema zako nipate nguvu,

Nikae nikupendeze mwokozi wangu,

shetani muovu kamwe asinipate.

Verse 3

Nilinde niwe imara na mwenye nguvu,

nisitumbukie tena katika dhambi,

Unionyeshe yaliyo ya heri kweli,

nipate kuishi kwa kumpendeza Bwana

Verse 4

Nawe uliye njia kweli na uzima,

niongoze vyema daima siku zote,

Uniangazie mwanga palipo giza,

nifkishe kwake Baba kwa neema yakon

Verse 5

Nakukaribisha Bwana moyoni mwangu,

nijarie ewe Bwana baraka yako,

Hata siku ya mwisho nitakuapia,

ni ile mbinguni kwenye heri milele.

Comments

Sign in to join the conversation

Share your thoughts on this hymn with the community.