Ninakupenda Mungu
Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary TimeThanksgiving
Chorus
Ninakupenda Mungu (wangu)
Ninakupenda wewe milele na milelen(Bwana) nitakutukuza
Pokea sifa zangu (Bwana)
Zinazotoka katika kinywa changu mimin(ndani) na moyoni mwangu *2n
Verse 2
Katika makusanyiko nitaziimba zaburi
Nitazitangaza sifa zako daima milele
Kwenye madhabahu yako nitaitoa sadaka
Ile ya kukupendeza ee Mungu Muumba wangu.
Verse 3
Umenitendea mengi, mema yasiyo idadi
Ninakushukuru Bwana, ee Baba Muumba wangu
Nikiyakumbuka yote, machozi yanimwagika
Ni machozi ya furaha, ni machozi ya upendo.
Verse 4
Usiniache ee Bwana, na wala usinitupe
Ukinitupa wewe, nani ataniokota
Ndiwe msitiri wangu, katika dunia hii
Dunia yenye mateso na yenye mahangaiko
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.