Chorus
Ningekuwa na mabawa, ningeruka hadi mbinguni
Ningekuwa na ufunguo, ningefungua mlango wakon{ Niingie nyumbani mwako, nikuimbie Mungu wangu
Katika makao yako, makao ya milele } *2
Verse 2
Malaika wanakuimbia nyimbo nzuri za furaha.
Makerubi hata maserafi wanasifu jina lako
Verse 3
Ningekuwa mimi ni bahari ningevuma kwa sauti
Ningekuwa mimi ni kengele ningelia usikie
Verse 4
Bwana mimi nitakuimbia siku za maisha yangu
Nitaimba sifa zako Bwana ili watu wasikie
Verse 5
Naamini kwamba siku moja nitafika mbele zako
Natamani sana kuja kwako kwenye raha ya milelen
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.