Ningelikuwa Kengele
Ningelikuwa ni kengele mimi ningelia usikie!
Ningelikuwa ni maua mimi ningechanua chanua
Ili niupambe uso wako ewe Mungu uliyeniumban(Tena mimi) ukanipatia akili na mali ili nikutumikien{ Naona fahari ninapotamka maneno haya,
Ninapotazama kwa jinsi ulivyonipenda mimi kupita upeo } *2
Umetamalaki Mungu (Mungu wangu),
Nikulipe nini Bwana (hakika)
Kila ninapotazama, wanadamu tulivyoumbika
Akili na maarifa (yote hayo)
Umetupatia Mungu (tazama)
Sisi viumbe pekee, utashi nao ukatujaza
Neema zako ni kuu (sana sana)
Kwa wanao wote Baba (hakika),
Mvua yako wainyesha hata kwa viumbe wenye dhambi
Shukurani ninatoa (mimi Bwana),
Kiumbe mnyonge Baba (naomba),
Wabariki mayatima, na wale wasio na uwezo
Comments
Sign in to join the conversation
Share your thoughts on this hymn with the community.