SectionsExitNitajisifia Udhaifu Wangu

Nitajisifia Udhaifu Wangu

Lent,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Lent,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary TimeExit
Chorus

Nitajisifia udhaifu wangu udhaifu wangu,

ili uweza wa Kristu ukae juu yangunmaana ninapokuwa dhaifu ndipo nilipo na nguvu x2

Verse 2

Sina budi kujisifia japo kuwa haipendezi,

lakini ninajizuia nisihesabiwe hatia,

bali nasema ukweli juu ya maono niliyopata.

Verse 3

Sababu ya mafunuo hayo nalipewa mwiba mwilini,

nikamsihi Mungu wangu jambo hili liniepuke,

naye akaniambia neema yangu pekee inatosha.

Verse 4

Napendezwa na udhaifu dharau taabu mateso,

nakuyavumilia yote hayo kwa ajili ya Kristu,

kwani uweza wa Kristu hutimia katika udhaifu.

Comments

Sign in to join the conversation

Share your thoughts on this hymn with the community.