SectionsEucharistNjia Ya Msalaba

Njia Ya Msalaba

LentEucharist
Verse 1

Umekosa nini we Yesu

Kushitakiwa bure kwa pilato

Mwenye kustahili hukumu

(Si wewe si wewe Bwana ni sisi) x2

Verse 2

Ole msalaba huo mzito

Apagazwa mwana mpenzi wa Mungu

Mwili waenea mateso

(Alipa alipa madhambi yetu) x2

Verse 3

Ona Muumba mbingu na nchi

Yupo chini mzigo wamwelemea

Na mtu kiumbe chake kwa ukali

(Ampiga ampiga bila huruma) x2

Verse 4

Huko njiani we Maria

Waonaje hali ya Mwanao

Ni damu tupu na vidonda

(Machozi machozi yamfumba macho) x2

Verse 5

Kwa Simon heri ya kweli

Mimi pia Yesu nisaidie

Kuchukua mzigo wa ukombozi

(Kuteswa kuteswa pamoja nawe) x2

Verse 6

Uso wa Yesu malaika

Bethlehemu walikuabudu

Bahati yake Veronica

(Kupangusa kupangusa Mfalme wanmbingu) x2

Verse 7

Wakimvuta huku na huku

Wauaji wanamchokesha bure

Chini wamtupa bado kwa nguvu

(Aibu aibu yao milele) x2

Verse 8

Wanawake waisraeli

Musilie kwa sababu hiyo

Muwalilie hao kwa dhambi

(Upanga upanga ni juu yao) x2

Verse 9

Mwokozi sasa ni ya tatu

Waanguka chini ya msalaba

Katika dhambi za ulegevu

(Nijue nijue kutubu hima) x2

Verse 10

Muje malaika wa mbingu

Funikeni mwiliwe kwa huruma

Vidonda vyake na utupu

(Askari askari wamemvua) x2

Verse 11

Hapo mkristu ushike moyo

Bwana wako alazwa msalabani

Mara miguu na mikono

(Yafungwa yafungwa kwa misumari) x2

Verse 12

Yesu mpenzi nakuabudu

Msalabani unapohangaika

Nchi yatetemeka kwa hofu

(Najua najua linaffa) x2

Mama Maria mtakatifu

Verse 13

Upokee maiti ya mwano

Tumemuua kwa dhambi zetu

(Twatubu twatubu kwake na kwako) x2

Verse 14

Pamoja nawe kaburini

Zika dhambi na ubaya wa moyo

Yesu tuwe Wakristu kweli

(Twakupa, twakupa sasa mapendo) x2

Verse 15

Katika Roho yangu, Bwana

Chora mateso niliyokutesa

Nisiyasahau madeni

(Na kazi na kazi ya kuokoka) x2

Comments

Sign in to join the conversation

Share your thoughts on this hymn with the community.